Hymns and Prayers

TWENDE KWA YESU

1. Twende kwa YESU mimi nawe,
Njia atwonya tuijue Imo chuoni na
Mwenyewe Hapa asema njoo.

Na furaha tutaiona Mioyo ikitakata sana
Kwako mwokozi kuonana Na milele kukaa.

2. Wana na waje atwambia Furahini
mkisikia, Ndiye mfalme wetu pia
Na tumtii njoo.

3. Wangojeani? Leo Yupo Sikiza sana
Asemepo Huruma zake zikwitapo
Ewe kijana njoo.

  • Hymn
  • 31,852 views