Namwamini Mungu Baba Mwenyezi, Muumba mbingu na nchi:
Na Yesu Kristo Mwana wake wa pekee, 
Bwana wetu, Aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,
Akazaliwa na Bikira Mariamu, akateswa zamani za Pontio Pilato, 
Akasulibiwa, akafa, akazikwa, akashuka kuzimu;
Siku ya tatu akafufuka, akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba Mwenyezi: Kutoka huko atakuja kuwahukumu watu walio hai na waliokufa.
Namwamini Roho Mtakatifu: Kanisa Takatifu Katoliko:
Ushirika wa Watakatifu: Ondoleo la dhambi: kufufuliwa kwa mwili. 
Na Uzima wa milele. 
AMINA.                            

