Hymns and Prayers

NDINYO DHAMANA

Ndiyo dhamana, Yesu wangu; hunipa furaha za mbingu;
mrithi wa wokovu wake, nimezawa kwa Roho yake.

Habari njema, raha yangu, Yesu ndiye Mwokozi wangu,
habari njema, raha yangu, Yesu ndiye Mwokozi wangu.

Kumsalimu moyo wangu, mara namwona raha yangu;
ananiletea malaika, wananilinda, taokoka.

Sina kinyume; nashukuru, mchana kutwa hujakwangu;
usiku kucha kuna nuru; Mwokozi wangu; ndimi huru.

Hali na mali anitwaa! Mara namwona anifaa, nami
nangoja kwa subira; akiniita, nije mara.

  • Hymn
  • 4,083 views