Hymns and Prayers

NATAKA NIMJUE YESU

Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
nijue pendo lake, na wokovu wake kamili.

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu,
nijue pendo lake, na wokovu wake kamili.

Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia,
anenapo kitabuni, kujidhihirisha kwangu.

Nataka nifahamu, na nizidi kupambanua, mapenzi
yake, nifanye yale yanayompendeza.

Nataka nikae naye, kwa mazungumzo zaidi,
nizidi kuwaonyesha, wengine wokovu wake.

  • Hymn
  • 16,677 views