Hymns and Prayers

KARIBU NA WEWE

Karibu na wewe, Mungu wangu; karibu zaidi, Bwana wangu.
Siku zote niwe, karibu na wewe, karibu zaidi Mungu wangu.

Mimi nasafiri Duniani, pa kupumzika sipaoni,
nilalapo niwe karibu na wewe, karibu zaidi Mungu wangu.

Na kwa nguvu zangu nikusifu; mwamba, uwe maji ya
Wokovu;Mashakani niwe karibu na wewe; karibu zaidi Mungu
wangu.

Na nyumbani mwa juu, Baba yangu, zikikoma hapa siku zangu,
kwa furaha niwe pamoja na wewe, karibu kabisa Mungu wangu.

  • Hymn
  • 18,109 views