Hymns and Prayers

NASKIA KUITWA

Nasikia kuitwa, na sauti yako,
Nikasafiwe kwa damu, ya kwangikwa kwako.

Nimesogea, Mtini pako, Unisafi kwa damu,
ya kwangikwa kwako.

Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu,
Ulivyonisafi taka, ni utimilivu.

Yesu hunijuvya; mapenzi, imani;
Tumai, amani, radhi, hapa na Mbinguni.

Huipa imara, kazi yake, ndani;
huongezeka neema, ashindwe Shetani.

Huishuhudia, Mioyo ya imani
Ya kuzipata ahadi, wakimuamini.

Napata wokovu, wema na neema;
Kwako Bwana nina nguvu, na haki daima.

  • Hymn
  • 12,047 views