Hymns and Prayers

MSALABANI PA MWOKOZI

Msalabani pa mwokozi hapo niliomba upozi
Akaniokoa mpenzi, Mwana wa MUNGU

Mwana wa MUNGU, Mwokozi wangu,
Akaniokoa mpenzi, Mwana wa MUNGU

Chini ya mti msumbufu, niliomba utakatifu
Alinikomboa kwa damu, Mwana wa MUNGU

Aliniokoa dhambini,Ikawa kunikaa ndani
Aliponifia mtini, Mwana wa MUNGU;

Damu ya YESU ya thamani, huniokoa Makosani
Huniendesha wokovuni, Mwana wa MUNGU

Hicho kijito cha gharama, leo jivike kwa kuzama,
Kwake uuone uzima, Mwana wa MUNGU.

  • Hymn
  • 5,481 views