Hymns and Prayers

YESU KWETU NI RAFIKI

1. Yesu kwetu ni rafiki Hwambiwa haja pia,
Tukiomba kwa babaye, Maombi asikia
Lakini twajikosesha Twajitweka vibaya,
Kwamba tulimwomba Mungu Dua angesikia.

2. Una dhiki na maojo, Huwezi kwendelea,
Haifai kufa moyo, Dua atasikia,
Hakuna mwingine Mwema Wakutuhurumia,
Atujua tu dhaifu, Maombi asikia

3. Je hunayo hata nguvu Huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa, Ujaparushwa pia,
Watu Wangekudharau, Wapendao Dunia
Hukwambata Mikononi Dua atasikia

  • Hymn
  • 22,416 views