Hymns and Prayers

KATIKA NEEMA YA YESU

1. Katika neema ya Yesu Nimeokolewa,
Nilipotea dhambini, Kipofu rohoni.

2. Bali neema ya Yesu Yanitosha Sana
Ilinifumbua Macho ikanifungua.

3. Nilikuwa mwenye Hofu Nilifungwa nazo,
Nimefunguliwa Sasa Kwa neema ya Yesu.

4. Nitamsifu Bwana Wangu Maishani mwote,
Kwani nina Ushirika Msalabani Mwake.

5. Tutakapofika Wote Mbinguni kwa Mungu
Tutashukuru neema Ya Yesu milele.

  • Hymn
  • 4,359 views