Hymns and Prayers

FURAHA KWA ULIMWENGU

1. Furaha kwa ulimwengu!
Bwana amekuja;
Nyote mkaribisheni,
Mioyo yenu na mpeni;
(Wote wanshangilie,)x2
Na wote, na wote wamshangilie.

2. Furaha kwake dunia!
Mwokozi ni Mfalme;
Bonde na mlima na mwamba,
Maji mitoni na shamba,
(Rudisheni sauti) x2,
Rudisheni, na rudisheni sauti.

3. Dhambi zisiongezeke,
Wala wahalifu;
Yuaja kutubariki,
Atuletea ushindi;
(Kuharibu dhambi,) x2
Na kuharibu, na kuharibu dhambi.

4. Atawala na neema,
Kwao mataifa;
Utukufu na waone,
Haki yake itendeke;
(Kwa upendo wake,)x2
Kwa upendo, na kwa upendo wake.

  • Hymn
  • 5,590 views