Hymns and Prayers

WAIMBA, SIKIZENI

1. Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni;
Wimbo wa tamu sana,Wa pendo zake Bwana;
"Duniani salama, Kwa wakosa rehema."
Sisi sote na twimbe, Nao wale wajumbe;
Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni.

2. Ndiye Bwana wa mbingu, Tangu milele Mungu,
Amezaliwa mwili, Mwana wa mwanamwali;
Ametoka enzini, Kuja ulimwenguni
Mwokozi atufie, Ili tusipotee,
Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni.

3. Seyidi wa amani, Ametoka Mbinguni,
Jua la haki, ndite, Atumulikiaye;
Amejivua enzi, Alivyo na mapenzi,
Ataka kutuponya, Kutuzalisha upya,
Waimba, sikizeni,Malaika mbinguni.

  • Hymn
  • 3,156 views