Hymns and Prayers

Nimehitaji Mwokozi

1. Nimehitaji Mwokozi
Awe nami daima;
Nataka mikono yake,
Kunizunguka sana.
Hofu rohoni sina, Aniongoza tena;
Sitanung'unika tena,Nimfuate daima.

2. Nimehitaji
Mwokozi, Sina
imani nyingi;
Atanifufusha moyo,
Wengine hawawezi.

3. Nimehitaji Mwokozi,
Mwendoni mwa maisha;
Katika mateso mengi,
Tena katika vita.

4. Nimehitaji Mwokozi,
Kiongozi njiani;
Kwa jicho aniongoze,
Ni'fike mbinguni.

  • Hymn
  • 7,174 views