Hymns and Prayers

DAMU IMEBUBUJIKA

1. Damu imebubujika, ni ya Imanweli
Wakioga wenye taka, husafiwa kweli.

2. Ilimpa kuushukuru mwivi mautini
Nami nisiye udhuru, yanisafi ndani.

3. Kondoo wa kuuawa, damu ina Nguvu
Wako wote kuokoka, kwa Utimilivu.

4. Bwana tangu Damu yako, kunisafi
Kale Nimeimba sifa zako,taimba milele.

5. Nikifa tazidi kwimba, sifa za Wokovu
Ulimi ujaponyamaa, vumbini mwa ufu.

6. Bwana, umenikirimu Nisiyestahili
Kwa damu yako, sehemu Ya mali ya kweli.

  • Hymn
  • 3,001 views