Hymns and Prayers

LIKO LANGO MOJA

1. Liko lango moja Wazi,Ni lango la Mbinguni,
Na wote Waingiao Watapata nafasi.
Lango ndiye Yesu Bwana Wote Waingie Kwake,
Lango! LangoLa Mbinguni ni wazi.

2. Yesu ndiye lango hili,hata sasa ni wazi, Kwa
wakubwa na wadogo, Tajiri na maskini.

3. Hii ni lango la raha, Ni lango la rehema,
Kila mtu apitayeHana majonzi tena.

4. Tukipita lango hili Tutatua mizigo
Tulichukua kwanza Tutavikwa uzima

5. Hima ndugu Tuingie lango halijafungwa
likifungwa mara moja halitafunguliwa.

  • Hymn
  • 41,240 views