Hymns and Prayers

SIONI HAYA KWA BWANA

1. Sioni haya kwa Bwana, Kwake nitang'ara!
Mti wake sitakana, Ni neno imara.

Msalaba ndio asili ya mema, Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima, Njoni kafurahini papo.

2. Kama kiti chake vivyo, Ni yake ahadi;
Alivyowekewa navyo, Kamwe, havirudi.

3. Bwana wangu, tena Mungu, Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu, Wala kunikana.

4. Atakiri langu jina, Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena, Mbinguni nikae.

  • Hymn
  • 16,365 views