Hymns and Prayers

OMBA UAM-KAPO

1. Omba uam-kapo, omba na m-chana,
Omba tena jioni, omba na usiku,
Roho yangu, uache matendo ya giza,
M-tumaini Yesu, omba kila mara.

2. Ndugu, uwe na nia kuombea watu,
Wapenzi na adui wakusumbuao
Na mimi faraghani huomba daima.
Na mahitaji Yangu Mungu hunijaza

3. Ukiwa huna chumba, omba faraghani,
Acha mashaka yote, M-fariji yupo,
Akae ndani yako Roho Mtakatifu,
Akufikishe kwake mbinguni kwa Baba.

4. Huna baraka nyingi, upendaye n-chi,
Umeamriwa hivi, tegemea Mungu,
Je, umefanya dhambi? Mwombe Bwana Yesu,
Umfurahie Yeye ndiye Mungu Mpenzi.

  • Hymn
  • 2,702 views