Hymns and Prayers

Yesu Nakupenda

1. Yesu nakupenda, U Mali yangu,
anasa za Dhambi sitaki kwangu;
Na Mwokozi aliyeniokoa,
Sasa nakupenda, kuzidi Pia.

2. Moyo umejaa Mapenzi tele,
kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai Wako ukanitolea,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

3. Ulipoangikwa Msalabani,
tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
sasa nakupenda, kuzidi pia

4. Niwapo hai, niwapo maiti,
kupendana nawe kamwe siachi;
Hari za kifo zikinienea,
sasa nakupenda, kuzidi pia.

5. Mawanda mazuri, na masikani,
niyatazamapo huko Mbinguni,
Tasema na taji nitakayovaa, sasa
nakupenda, kuzidi pia.

  • Hymn
  • 5,684 views