Hymns and Prayers

TWAE WANGU UZIMA

1.Twae wangu uzima, Sadaka ya daima; Twae saa na siku, Zikutukuze huku.

2.Twae mikono nayo, Ifanye upendavyo, Twae yangu miguu, kwa wongozi wako tu.

3.Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu; Itwae na midomo, Ijae neno lako.

4.Twae dhambi pia, Na yote ya dunia; Twae yangu hekima, Upendavyo tumia.

5.Nia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu; Twae moyo; ni wako, Uwe makazi yako.

6.Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu; Twae kabisa nafsi, Niwe wako halisi.

  • Hymn
  • 3,045 views