Hymns and Prayers

CHA KUTUMAINI

1. Cha kutumaini sina Ila damu yake Yesu
Sina wema wa kutosha dhambi zangu kuziosha.
Kwake Yesu nasimama, ndiye mwamba ni salama,
Kwake Yesu nasimama, ndiye mwamba ni salama

2. Njia yangu iwe ndefu yeye hunipa wokovu
Mawimbi Yakinipiga nguvu zake ndizo nanga.

3. Damu yake na sadaka nategemea daima
Yote chini yakiisha mwokozi atanitosha.

4. Nikiitwa Hukumuni Moyoni nina amani
Nikivikwa haki yake Sina hofu mbele zake.

  • Hymn
  • 39,071 views